LyricFind Logo
LyricFind Logo
Profile image icon
Lyric cover art

Kimbilio Langu

Apple Music logo
Deezer logo
Spotify logo
Lyrics
Kwa Mungu nitakimbia niko na hofu nyingi sana
Roho yangu imechoka moyo umekufa ganzi
Nisalimishe kwa kweli ukanifanye imara
Hakika wewe ni ngome pahali salama kabisa

Kimbilio langu ni wewe msaada wangu ni wewe
Usiniondokee Baba wacha nitegemee wewe
Maadui wanashangaa jinsi unavyonihifadhi
Kimbilio langu ni wewe salama ndani mwako Mimi

Usinifiche uso wako nitafutapo uso wako
Nisamehe kosa zangu nami nijue njia zako
Kwa majivuno maadui wamenizunguka kweli
Lakini mikononi mwako nahisi hakuna hatari

Umeniinua juu ya jiwe miguu yangu haina tetemeko
Na nyimbo mpya imenijia midomoni kuna ushuhuda
Kwa upendo wako wa daima umeniita mwana wako
Ndani yako nasimama niko huru sina deni tena

Kimbilio langu ni wewe msaada wangu ni wewe
Usiniondokee Baba wacha nitegemee wewe
Maadui wanashangaa jinsi unavyonihifadhi
Kimbilio langu ni wewe salama ndani mwako Mimi

Umenibeba katika dhoruba za maisha na mateso
Umeniponya roho yangu kwa wema ambao hauna kipimo
Kabla ya maneno yangu kutoka moyoni umeshajua
Hakika upendo wako haufananishwi na maajabu yoyote

WRITERS

Rev. Nicholas Munyao

PUBLISHERS

Lyrics © O/B/O DistroKid

Share icon and text

Share


See A Problem With Something?

Lyrics

Other